Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Vyama vya ushirika vyatakiwa kujiendesha kiuchumi

$
0
0

Na Khamisuu Abdallah
VYAMA vya ushirika vinapaswa kuimarishwa na kuendeshwa kiuchumi na kibiashara ili kuviongezea uwezo wa kustahamili misukosuko ya kiuchumi.

Akitoa taarifa maalum ya Serikali, katika kuadhimisha siku ya ushirika duniani inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya mwazo ya Mwezi Julai kila mwaka Ofisini kwake Mwanakwerekwe, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman alisema kuna haja ya kuweka mikakati ya uanzishaji wa vyama hivyo vilivyokuwa madhubuti vya uzalishaji mali na utoaji huduma katika nyanja zote za kiuchumi, ili kuongeza fursa za ajira binafsi zenye heshima kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Waziri Haroun alisema kuwa kuadhimisha siku hiyo, vyama vya ushirika virudishe hadhi yake na viwe taasisi huru za kisheria zenye demokrasia na uwezo wa kutoa maamuzi na kuyatekeleza ili kukidhi mahitaji ya wanachama wake kwa kuwashirikisha kikamilifu katika harakati za kumiliki rasmi mali za nchi.

Aidha alisema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kupata fursa ya kutafakari na kukumbushana mchango na umuhimu wa sekta ya ushirika nchini katika kuzalisha ajira binafsi kwa makundi tofauti hasa kwa wanawake na vijana.

"Lengo kuu la maadhimisho haya ni kupata fursa ya kutafakari na kukumbushana michango na umuhimu wa sekta ya ushirika hapa Zanzibar katika kuzalisha ajira binafsi kwa makundi tofauti hasa kwa akinamama na vijana, kuongeza kipato na kupunguza umasikini kwa wananchi wote walioko mjini na vijijini" alisema Waziri Haroun.

Akizungumzia juu ya ujumbe wa siku ya Ushirika Duniani mwaka huu ambao unasema "Vyama vya Ushirika vibaki imara wakati wa Majanga na Misukosuko" alisema kuwa unalenga kuunganisha harakati za maendeleo ya sekta ya Ushirika Zanzibar na maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayoagiza kuanzishwa vyama hivyo kwenye nyanja zote za kiuchumi duniani.

Waziri huyo aliwasihi wanaushirika mbalimbali nchini kuviimarisha vyama vyao kwa kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuchumi zilizokubaliwa.

Pia aliwashauri viongozi kuzidisha uadilifu katika rasilimali za wananchi zilizowekwa kwenye vyama hivyo ili kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa kuwa na vyama imara vyenye uwezo wa kutetea maslahi ya wanachama wakati wa majanga.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>