Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

17 Wafa Ajalini.

$
0
0
Na Waandishi wetu
WATU 17 wamefariki katika ajali mbaya za barabarani zilizotokea Mkoani Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma jana.

Katika ajali ya kwanza iliyotokea jijini Dar es Salaam iliwahusisha wapanda pikipiki (bodaboda) ambao walikuwa wamepakizana watu watatu maarufu mshikaki.

Ajali hiyo ilitokea barabara ya Pugu, ambapo dereva wa pikipiki hiyo akiwa na abiria wake alishindwa kuidhibiti pikipiki yake na kuingia mfunguni mwa gari na kufariki papo hapo.

Ajali nyengine ilitokea mkoani Dodoma wilayani Chamwino ambapo watu sita walifariki na wengine 35 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori lililopakia mahindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, David Misime alisema gari hilo linalomilikiwa na kampuni ya Alsaid lilikuwa likitokea Dar es Salaam ambapo lilipofika eneo la Chamwino liligongana na gari lililopakia mahindi.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi.

Na huko mkoani Mbeya watu wanane walifariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.

Ajali hiyo iliihusisha daladala iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Majengo-Uyole.

Katika matukio mengine, Fatuma Kitima, anaripoti kwamba watu watano wamekufa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam, likiwemo la mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Chacha Marwa (48) kujinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 22 mwaka huu katika eneo la Kivule Nyanyandu.

Alisema sababu za kujinyonga bado hazijafahamika, na kaka wa marehemu alidai kuwa enzi za uhai wake alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya akili.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya taifa Muhimbili na upelelezi bado unaendelea.

Katika tukio la pili,mwanamme asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri ka ti ya (15-20) maiti yake ilikutwa ikiwa imelala katika eneo la Gongo la Mboto huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

Tukio hilo lilitokea Septemba 22 mwaka huu na kueleza kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa marehemu enzi za uhai wake alikuwa ni dereva wa bodaboda na huenda alichukuliwa na watu wasiofahamika eneo jingine hatimaye kuporwa pikipiki yake ambayo haijasomeka namba hatimaye kumtupa eneo hilo.

Katika tukio jingine, huko katika barabara ya Nyerere eneo la Vingunguti gari namba T216 CLL aina ya Volvo yenye Trela namba T 148 BEN ikiendeshwa na Abdalah Kasimu(25) mkazi wa Yombo Dovya akiwa amebeba mbolea mali ya kampuni ya Chohen alipofika Tazara Vingunguti akikata kona aligongwa kwa nyuma na gari namba T 415 AYB aina ya Vits na kusababishiwa kifo.

Wakati huo huo naye dereva wa pikipiki Koba Ramadhani (27) mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani amefariki dunia baada ya kugongwa na trekta namba T 811 AOK aina ya Masey Ferguson mali ya manispaa ya Kinondoni ikiendeshwa na Hamad Ally.

Katika hatua nyingine mwendesha pikipiki asiyefahamika mwenye namba T 250 BNR aina ya Skymark,amefariki dunia baada ya kugongwa na gari namba T 292 BWU ikiendeshwa na Shedrack Wililo(32)mkazi wa Bahari Beach.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema tukio hilo lilitokea Septemba 22 mwaka huu katika shule ya sekondari Makongo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>