Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Waliouawa Kenya 69. Magaidi Wajichoma Moto.

$
0
0
NAIROBI, Kenya
MOSHI mkubwa, milio ya risasi na miripuko ilisikika jana katika jengo la Westgate ambako wanamgmbo wa Al Shabaab wameteka jengo hilo pamoja na kuwashikilia mateka Wakenya.

Waziri wa Usalama wa ndani,Joseph Ole Lenku, alisema vikosi vya usalama vimedhibiti jengo hilo kutoka nje na ndani na kwamba ni mateka wachache walosalia katika jengo hilo.

Serikali imesema watu 62 wameuawa lakini shirika la Msalaba Mwekundu limesema idadi hiyo ni 69 wakiwemo raia wanne wa Uingereza na wanajeshi wawili.

Serikali ya Uingereza imesema raia wake Ross Langdon ameuawa akiwa pamoja na mchumba wake, raia wa Uholanzi, Elif Yavuz ambae ana ujauzito wa kujifungua.

Westgate ni jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa karibia 80.

Habari zinasema washambulia watano ni raia wa Marekani na wawili ni Waingereza na washambuliaji wote ni wanaume ingawa wengine wamevalia mavazi ya kike.

Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo lakini hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.

Wapiganaji wa Al Shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani.

Inaarifiwa kulikuwa na maiti 10 katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.

Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wako ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na miripuko ilisikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.

Harakati za kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.

Rais Uhuru Kenyatta amesema jeshi linajitahidi kuhakikisha linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.

Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria.

Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni tete katika eneo la shambulizi.

Awali jeshi la Kenya lilisema limedhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.

Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>