Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Basi Latekwa kwa Mawe, Mapanga. Abiria Waporwa Wajeruhiwa.

$
0
0
Na.Kadama Malunde, Shinyanga
WATU wasiojulikana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mawe na mapanga wameteka magari mawili likiwemo basi la Nkamba’s kisha kupora fedha na simu za abiria na kujeruhi sita usiku wa kuamkia jana katika daraja la 54 katika barabara ya Shinyanga kulekea Mwanza.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangalla tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku katika daraja hilo la 54 kijiji cha Buchambi kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu mkoani hapa,ambapo watu hao wakiwa na mawe na mapanga walitega mawe barabarani kisha kuyateka magari mawili.

Aliyataja magari yaliyotekwa kuwa ni pamoja na basi la kampuni ya Nkamba’s lenye namba za usajili T610 ARR scania pamoja na gari lenye namba za usajili T722 CKZ aina ya Fuso ambalo halijajulikana mmiliki wake,yote yakitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.

Kamanda Mangalla alisema katika tukio hilo abiria walinyang’anywa simu na fedha ambazo hazijajulikana idadi wala thamani yake, huku abiria 6 wakiwemo wanawake wanne na wanaumme wawili wakijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo tayari wameshapatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Aidha kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi zitakazopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa hao.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>