Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mradi wa Maji Jimbo la Kikwajuni wamalizika Awamu ya Kwanza kwa Uchimbaji Kisima.

$
0
0
Mtaalamu wa Uchimbaji wa Visima kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Mohammed Abdalla , akitowa maelezo baada ya kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa Jimbo la Kikwajuni la Uchimbaji wa Kisiwa kwa awamu ya kwanza,, Mbunge wa jimbo hilo Hamad Masauni akimsikiliza baada ya kutembelea kisima hicho kilioko katika eneo la Kaburi kokombe.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Masauni,akizungumza na Waandishi wa habari.kuhusu mradi huu wa maji kwa jimbo lake ambao utaondosha matatizo hayo iukiwa umekamilika kwa hatu ya mwazo kwa uchimbaji wa kisima katika eneo la Kaburikikombe na kina uwezo wa kutowa maji lita 60 elfa kwa saa , na kuwa na uhakika wa kuondoa tatizo hilo.hatua iliobaki ni ya awamu ya pili kutandika mabomba kutoka eneo la kaburi kikombe hadi kilimani mnara wa mbao kwa ajili ya kuwafikia wananchi wa jimbo lake.

Kisima cha Maji kwaajili ya Jimbo la Kikwajuni kikiwa katika hatua ya mwisho ya uchimbaji wake na kutowa maji lita 60 elfu kwa saa.
Mtaalamu wa uchimbaji wa Visima kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA. Mohammed Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari kutokana na mafanikio ya hatu ya kwanza ya uchimbaji wa kisima hicho kutokana na ushirikiono na ZAWA na Mbunge wa Kikwajuni katika mradi huomkubwa wa usambazaji maji na kuondoa tatizo hilo katika jimbo la kikwajuni.
Mbunge wa Kikwajuni Hamad Masauni akiwaonesha waandishi wa habari sehemu litakalowekwa tangi la maji katika mnara wa mbao kilimani kwa ajili ya kutowa huduma za usambazaji maji kwa jimbo lake  na kuondoa tatizo hilo linalolikabidhi kwa muda mrefu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>