Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wawakilishi waiomba Serikali kununua mashine ya DNA

$
0
0
Na Khamisuu Abdallah
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameiomba Serikali kuhakikisha kifaa cha DNA kinapatikana ndani ya muda mfupi kwa lengo la kuondoa changamoto iliyokuwepo sasa kwa kukosekana kwa kifaa hicho  ambapo kesi nyingi za udhalilishaji hazipatiwi ufumbuzi.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa viti maalum ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mhe: Mgeni Hassan Juma wakati akifanya majumuisho ya hoja binafsi aliyoiwasilisha barazani hapo.

Aidha alisema wajumbe hao walipendekeza  kutokana na kuongezeka kwa mimba za utotoni kifaa hicho kitaweza kusaidia  kuwatambua wahusika wa matukio hayo bila ya usumbufu wa aina yoyote.

Aidha Mhe. Mgeni alisema wajumbe hao walisema suala la rushwa ndilo linachangia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza vitendo hivyo ndani ya jamii na watahakikisha kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha swala hilo linapigwa vita na kupatikana haki ya kisheria.

Alisema  wajumbe hao pia walipendekeza sulala la udhalilishaji lisiachiwe serikali pekee na badala yake wajumbe, taasisi mbalimbali zina uwezo wa kupeleka miswaada barazani ambayo itaweza kuisaidia serikali katika kulifanyia kazi swala la udhalilishaji hapa nchini.

Hata hivyo wajumbe hao walipendekeza azimio namba 7 kuwa serikali  ifanyie mapitio sheria ya mtoto kwa utekelezaji wa hoja za jamii kwa matatizo ya watoto yanayowakwaza ili vitendo hivyo viweze kuondoka hapa nchini.

Wajumbe hao walisema suala la upatanishi linalofanywa na wazee pamoja na wafanyaji wa vitendo hivyo katika kumaliza kesi kwa  kumalizana wenyewe bila kufika katika vyombo vya mahakama watu wamelipiga vita na  kuomba kuwekwa kwa sheria maalum ambayo itamchukulia hatua mzee yoyote atakaepinga sheria hiyo.


Alisema kuwa katika majumuisho hayo pia wajumbe hao walipendekeza kuingizwa kwa elimu ya udhalilishaji katika mitaala sambamba na kuelimisha jamii juu ya mambo hayo.

Hata hivyo wajumbe hao waliiomba Serikali kundosha vipindi vilitakavyoweza kuondoa maadili kwa wazanzibari hasa kwa watoto katika televisioni na redio.

Sambamba na hayo alisema  wajumbe hao waliiomba serikali kutoa ripoti ya udhalilishaji kwa kila mwaka ambapo itawasilisha kutoka Wizara ya Ustawi wa jamii vijana na watoto.

Pia wajumbe hao waliiomba serikali kuziimarisha mahakama kwa kuzitilia mkazo kesi za watoto kwa kusikiliza kwa muda mfupi.


wajumbe wote walimunga mkoni mazimio yote ambapo azimio moja kuwepo kwa vikao kati ya mwanasheria mkuu waziri wakatiba na sheria ili kuweka


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>