Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wazee wa Kimasai wataka washirikishwe vita dhidi ya ukeketaji

$
0
0
Na Amina Omari, Kilindi 
WAZEE wa kimila wa kabila la kimasai, wameitaka serikali kuwashirikisha katika vita dhidi ya ukeketaji wasichana na ndoa za umri mdogo.

Ushauri huo umetolewa na kiongozi wa kimila wa jamii hiyo wilayani Kilindi mkoani Tanga,Simon Oleamushana, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema vita dhidi ya ukeketaji vitamalizwa iwapo viongozi wa jamii hiyo watashirikishwa kwa ukamilifu wake.

Alisema vita hivyo havitafanikiwa kwa kuwashirika watu wasiohusika na badala yake kusikingizia kuwa wamasai hawataki kuachana na mila hizo.

“Najua serikali inachukua juhudi kubwa kutaka kutokomeza mila za ukeketaji na mimba za utotoni lakini wanachokosea hawatushirikishi sisi wazee wa kimila ambao ndio tuna jukumu la kuleta mabadiliko katika jamii yetu,”alisema.

Nae Raheli Ngushai alisema jamii hiyo imeonekana kusahauliwa katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu na afya hali inayosababisha kuendelea kushiriki vitendo vya mila.

Hata hivyo, aliyashukuru mashirika ya kijamii likiwemo AMREF kwa kujitolea kuwaelimisha madhara ya ukeketaji kwa wasichana.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>