Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JK ala krismasi na yatima

$
0
0
Na Kiza Sungura, MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa kilo 1,200 za mchele, lita 220 za mafuta na mbuzi 25 kama  zawadi yake ya krismasi kwa makundi maalum.

Zawadi hizo zilikabidhiwa jana na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete katika hafla fupi iliyofanyika uwanja wa mahabusu ya watoto jijini Dar es salaam.

Alisema Rais Kikwete ametoa zawadi hiyo ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na watato walioko katika mkinzano na sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania wengine kusherekea sikukuu hiyo.
Alisema mbali ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam, pia alitoa kwa makundi mengine katika mikoa mbali mbali nchini.

Alisema kwa upande wa Dar es Salaamametao msaada kwa vituo 11 vinavyosaidia huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza.

Vituo vilivyofaidika ni kituo cha watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, makazi ya watoto Kurasini, Temeke, makazi ya watoto yatima Msimbazi, kituo cha kwetu Mbagala, kituo cha yatima na kituo cha chakuwama.


Vingine ni mahabusu ya watoto, makazi ya watoto yatima Mburahati, kituo cha tuwapende watoto Bunju, makazi ya wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe.

Alisema kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es Salaamzawadi zao watapatiwa katika maeneo yao.

Alivitaja vituo vya nje ya Dar es Salaam kuwa ni kituo cha Mabaoni Chake Ckale Pemba, kituo cha wazee Welezo Unguja, mahabusu ya wototo Moshi na makazi ya wazee wasiojiweza Sukamaela Singida.

Vingine ni makazi ya wasiojiweza Bukumbi na makazi ya wazee wasiojiweza Msufini, Tanga.

 Alisema Rais ametoa zawadi hizo kwa kutambua kuwa watoto na wazee wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika kusherehekea sikukuu hiyo vyema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>