Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashillah amesema Kikao cha Bunge hilo litaanza kwa hatua ya kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho kwa ajili ya kupanga kanuni za kuendesha Kikao na kufanya uchaguzi
Amesema katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa Bunge atapigiwa kura na wajumbe na Makamo Mwenyekiti wake, ili kuanza kwa kuendesha Kikao cha Bunge la Maalum la Katiba Mpya ya Tanzania kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba hiyo ili kuichangia na kupata Katiba iliokuwa Safi
Amesema Kikao hicho kitakuwa chini ya Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Yahya Khamis Hamad , na kufanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho
Amesema taratibu zote za Kikao hicho zimekamilika na kinachusubiriwa ni kuanza kwa Kikao hicho cha Historia kwa Tanzania kupitisha kwa Katiba ya Tanzania ni mabadiliko ya Kwanza tangu Tanzania kupata Uhuru.
Tayari takribani Wajumbe wate wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania Wameshawasili Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Bunge la Katiba Tanzania.
Mji wa Dodoma ukiwa katika uchangamfu wa wageni mbalimbali waliofika kushuhudia mkutano huo wa historia kwa Tanzania kupitisha Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wananchi wa Tanzania wataangalia Bunge hilo Maalum kupitika katika Vyombo vya habari mbalimbali Tanzania na kuoneshwa katika TV ya Taifa ya TBC, na Tv nyegine wakati wa saa nane mchana zitakapoaza shughuli hizo leo huko Dodoma.
Wananchi wa Tanzania wataangalia Bunge hilo Maalum kupitika katika Vyombo vya habari mbalimbali Tanzania na kuoneshwa katika TV ya Taifa ya TBC, na Tv nyegine wakati wa saa nane mchana zitakapoaza shughuli hizo leo huko Dodoma.