Na Kunze Mswanyama, DSM
NAIBU Waziri wa zamani wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,Dk.James Wanyancha,amewataka wabunge wa bunge maalum la katiba, kuhakikisha wanatetea maslahi ya umma na kuacha kulumbana juu ya maslahi ya vyama au taasisi zilizowachagua.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dk.Wanyancha, alisema kwa sasa taifa liko njia panda kutokana na mapendekezo ya serikali moja,mbili na wengine wakitaka serikali tatu jambo ambalo anahisi ndiyo litaleta shida kwenye bunge hilo .
“Nawaomba wabunge hawa wasijadili kwa siasa, watatuletea shida kubwa baadae kwani tume ziliundwa nyingi zote zilitaka serikali tatu,tume ya Robert Kisanga na Francis Nyalali zote zilielekeza huko laikini ilipingwa sana , sasa mambo yamegeuka na hatimae naamini itapita,” alisema.
“Wakati wa serikali tatu umefika nawaomba wabunge wote wakubaliane na matakwa ya wananchi kwa kuwa hayo ni mawazo yao, katiba ni mali ya Watanzania wote siyo ya baadhi tu, hivyo nawaomba wasichakachue mawazo ya Watanzania,” alisema.
Akizungumzia kuhusu vita dhidi ya ujangili,Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Serengeti, alimuomba rais Kikwete awataje mapapa 40 wa ujangili aliosema anawatambua ili kuhakikisha vita hiyo vinapiganwa hadharani lakini kwa mafanikio makubwa.
Akiwa Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita,Rais Kikwete aliiambia dunia kupitia mkutano ulioandaliwa na motto wa Malikia wa Uingereza na kuhusisha nchi zaidi na 30 na mashirika 13 ya kimataifa kuwa,tayari serikali imebaini mtandao mpana wa majAngili hao na kwamba jitihada zinafanyika kuuzima kabisa.
“Sidhani kama rais anaogopa kuwataja kwa kuwa yeye analindwa na sheria, awataje ili tuwajue wahujumu wa rasilimali zetu, tunahangaika kupiga kelele za majngili, oparesheni nyingi kumbe rais anawajua majangili hao lakini hataki kuwataja, naomba awaambie Watanzania ili walinde rasilimali zao kwa nguvu zote,” alisema.
Alisema kama serikali haitakuwa radhi kupambana na majngil, vita hivyo havitakwisha.
Kuhusu wafanyakazi ambao wanatakiwa kustaafu, aliwataka kujiandaa mapema kwani hakuna namna itakayomfanya mfanyakazi asistaafu utumishi wake.
Alisema kustaafu siyo tiketi ya kifo kwani watumishi wengi hudhani akishastaafu tu ndiyo itakuwa mwisho wake wa kuishi duniani.
Kuhusu siasa, alisema anatarajia kuutarifu umma kuhusiana na matarajio yake ya baadae kisiasa ambapo muda ukifika atajua kama arudi kwenye siasa au la.