Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Nyumba zaidi ya 50 kuvunjwa Tunguu

$
0
0
Na Hafsa Golo
ZAIDI ya nyumba 50 na misingi zilizojengwa katika kijiji cha Tunguu zinatarajiwa kuvunjwa na serikali kufuatia uvamizi uliofanywa na wananchi. 

Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji,Dk. Mohammed Juma,  alisema eneo hilo tayari limepimwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, skuli,taasisi za serikali na binafsi.

Alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wananchi cha kuvamia na kujenga nyumba za kuishi  hakiwezi kufumbiwa macho.

Alisema watendaji wanaosimamia masuala ya ardhi wamekusudia kutekeleza kwa vitendo majukumu yao na kwamba nyumba hizo zitavunjwa.

"Baadhi ya wananchi wamekuwa wakijaribu kama serikali itaweza kufanya maamuzi au tutafanya nini, tunasema tumebadilika tutazivunja nyumba hizi kwa sababu wahusika wamevamia,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ardhi na Usajili, Januari Fusi, alisema serikali haikurupuki katika mipango yake hata kama utekelezaji wake utachukua muda mrefu.

Aidha alisema suala la kuwaondosha watu wote waliovamia linasimamiwa na ngazi zote za serikali hivyo hakutokuwa na maamuzi mengine.


Alisema serikali imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kutoa taaluma kwa wananchi juu ya uvamizi wa eneo hilo ambapo kwa hatua ya awali walitoa matangazo kupitia vyombo vya habari.

Mmoja ya mwananchi ambae ni mkaazi wa eneo hilo, Eduu Juma, alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba pamoja na taratibu zinazoendelea kuchukuliwa na serikali lakini ni vyema serikali ikafanya mazungumzo na wakaazi wa eneo hilo ili waweze kupata ukweli wa umiliki wao.

"Mimi sijavamia naishi hapa miaka 40 sasa na eneo hili nimerisi kutoka kwa marehemu mume wangu leo wanataka tuhame niende wapi na watoto hawa lazima serikali ituhurumie"alisema.


Naye Hassan Mkulima alisema kwamba serikali haitendi haki kwa kuwa eneo hilo wanalimiki kisheria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles