Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi wampiga risasi mwanajeshi JKT

$
0
0
Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
POLISI mkoani hapa wamemuua kwa kumpiga risasi askari wa jeshi la kujenga taifa (JKT) kikosi cha Oljoro na kumjeruhi mwingine katika mapambano yaliyotokea eneo la kwa Mromboo,baada ya marehemu kudaiwa kumpokonya askari polisi magazine iliyokuwa kwenye silaha aina ya SMG.

Marehemu ametambulika kwa jina la Joram Mnyakule (24)mwenyeji wa Kigoma huku majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru akiendelea kupatiwa matibabu  bado hajatambulika.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,ambaye aliomba kutotajwa jina lake akihofia usalama wake, tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 4:00 usiku,katika eneo hilo la kwa Morombo ,ambapo marehemu akiwa na wenzake 20 walivamia eneo hilo na kutembeza kichapo kwa raia yeyote wanayekutana naye wakidai wanasaka sare zao  zilizoibiwa.

Hata hivyo, polisi wa doria walipata taarifa kuhusiana na tukio hilo na kufika eneo hilo,ambapo walianza kuwasihi wanajeshi kuacha vurugu lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida ,wanajeshi hao waliwageuzia kibao na kuanza kuwashambulika huku baadhi yaowakitaka hata kuwanyang'anya silaha.


Taarifa zinadai kwamba polisi walipofika eneo hilo kwa lengo la kuzuia ghasia zilizokuwa zikiendeshwa na watu hao wanaosadikiwa ni wanajeshi waliokuwa wakimsaka kibaka anayedaiwa kukwapua mfuko uliokuwa na sare za mmoja wa wanajeshi hao,ndipo wanajeshi hao walipowageuzia kibao polisi na kuanza kuwashambulia.

Hali hiyo ilichukua takribani dakika 20 wakivutana huku marehemu akichukua jukumu la kunyang'anya mmoja wa askari polisi 'magazine' iliyokuwa kwenye silaha aina ya SMG na kutaka kutokomea nayo,ndipo askari polisi mmoja alipomfyatulia risasi mgongoni na kupoteza maisha na kumjeruhi mwingine.

Hali hiyo ilisababisha wanajeshi wengine waliokuwa eneo hilo kuanza kutawanyika wakihofia usalama wao.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipotafutwa kuzunngumzia tukio tukio hilo hakupatikana,hata hivyo baadhi ya polisi walioshuhudia walithibitisha na kueleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>