Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ukosefu wa vipimo vya Vinasaba kisiwe kisingizio cha kuwaachia wanaodhalilisha wanawake

$
0
0
Na Haji Nassor, PEMBA
VYOMBO vya sheria nchini, wametakiwa kuacha kisingizio cha ukosefu wa kipimo cha vinasaba ‘DNA’ na kuwaachia huru wanaowadhalilisha wanawake na watoto, ikiwa ni pamoja na wabakaji.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa Mipango wilaya ya Chakechake Pemba, Kassim Ali Omar skuli ya Madungu alipokuwa akifungua kongamano la siku moja, la kupinga ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na jumuia ya kimataifa ya UNA.
 Alisema sio busara kwa vyombo hivyo, kupata kichaka cha ukosefu wa kipimo hicho, na hatimae kuwaacha watoto na wanawake wakiwa wamedhalilika na wakosaji kudunda mitaani.
 Alieleza kuwa zipo kesi kadhaa za ubakaji, kutorosha na hata za watoto wa kike kupewa ujauzito, na ushahidi wote kukamilika, ingawa ukosefu wa kipimo hicho husababisha wakosaji kuwa huru.


 “Sasa kama kuna kesi ya ujauzito, eti mtuhumiwa achiwe huru mpaka mtoto wa kike ajifungue, na kuchuliwa vipimo vya ‘DNA’ sasa kilichozaliwa kikifa ndio hakuna kesi’’,alihoji Afisa mipango huyo.
 Katika hatua nyengine ameitaka jamii kushirikiana vyema na  vyombo vya sheria, serikali kuwa kitu kimoja, katika kutafuta njia ya kuzitokomeza kesi hizo.
 Akizungumza kwenye mdahalo huo, Mkuu wa Idara ya wanawake na watoto wa Wizara ya uwezeshaji, ustawi wa Jamii maendeleo ya wanawake na watoto Pemba, Sara Khamis Salim alisema wazazi wamekuwa wakijitahidi katika malezi, ingawa watoto hubuni njia ya kuwatoroka.
 Nae Afisa mkuu wa dawati la jinsia na watoto la Polisi mkoa wa kusini Pemba Asha Talib, alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa katika kutomeza kesi za udhalilishaji wa kijinsia.
 Alieleza kuwa jeshi la Polisi kwa makusudi limeanzisha madawati 417 Tanzania, ili kuhakikisha wanawake na watoto wanaishi bila ya ukatili, ingawa jamii imekuwa ikiviza nguvu hizo kwa kutokuwa tayari kutoa ushirikiano.
 Alifafanua kuwa, hilohujitokeza hasa, wakati wakosaji wanapokua na uhusiano wa kidamu na waathirika wa matendo hayo, ambapo jamii huyafumbia macho.
 Kongamano hilo ambalo limewashirikisha wanafunzi wa vilabu vya vijana skuli za Piki, Shamiani, Wawi mambo mbali mbali yalifanyika ikiwa na pamoja na utenzi na mchezo wa kuigiza.

 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>