Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mkoani Pemba washajiishwa kujifunza Kompyuta

$
0
0
Habiba Zarali, PEMBA.   
Wananchi Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba wameshajiishwa kujifunza kompyuta, ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya teknolojia Ulimwenguni.
 Akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya kompyuta katika mahafali ya kituo cha Uweleni , Afisa elimu Wilaya ya Mkoani Seif Mohamed Seif amesema taaluma hiyo itawafungulia vijana milango ya ajira katika sekta za umma na binafsi na hata kujiajiri wenyewe.
 Aidha alisema kuwa vijana hawana budi kuchangamkia fursa ya kuwepo kwa kituo hicho  kwani kimewapunguzia usumbufu wa kufuata mafunzo hayo katika wilaya ya Chake chake.
 “wananchi eleweni kuwa darasa hili ni mkombozi kwa Wilaya ya Mkoani kwani kabla ya kuanzishwa mulikuwa mukilifuatilia huduma hii Chake na mukipata usumbufu mkubwa sana,alisema afisa huyo.
 Alieleza kuwa wakati umefika wa kuwa na wataalamu wa fani zote ambazo haziwezi kukamilika bila yakuwa na ujuzi wa kompyuta.
“Kompyuta ndio roho ya  elimu inawezesha kufanya kila jambo,”alisisitiza.
 Hata hivyo aliwataka wazazi kutowa mashirikiano ya dhati, ili kuhakikisha kituo hicho kinaendelea,sambamba na kuwataka wahitimu hao kuutumia vyema utaalamu waloupata, ili waweze kuleta maendeleo kwao na nchi kwa ujumla.
 Kwa upande wake Mkuu wa taaluma skuli ya Sekondari Uweleni maalim Mohammed Ussi aliwataka wananchi wa Mkoani kuunganisha nguvu zao za pamoja, ili kukamilisha ujenzi wa jengo jipya ambalo litakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kutoa mafunzo hayo.
Kamatulivyounganisha nguvu zetu za pamoja na tukakamilisha jengo hili la ghorofa, basi pia tunaweza kulimaliza jengo letu tulilolianzisha na kuweza kutowa nafasi kubwa zaidi.
Aidha aliwaasa wanafunzi wa kidato cha sita skulini hapo kuitumia fursa hiyo kwa kujisomea bure ,jambo ambalo kwao ni la faraja katika masomo yaowatakapoingia vyuoni.
 Nae mwalimu wa mafunzo hayo kwa niaba ya walimu wenzake alisema kituo hicho kilianza kutowa mafunzo hayo mnamo mwaka 2006 kwa wanafunzi wa kidato cha sita na waalimu wazalendo ambapo sasa ndio wanaoekiendeleza kituo  hicho,ambapo alisema mwaka 2008 kituo kilitowa huduma kwa wananchi wa wilaya nzima

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles