Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kivuko mto Kilombero chasombwa na maji

$
0
0
Na Judith Mpalanzi, Kilombero
Kivuko cha mto Kilombero kinachotumika kuvusha watu na mizigo kutoka na kwenda Ulanga, kimesombwa na maji na kumlazimu Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kilombero na Ulanga, Francis Mitti, kupiga marufuku shughuli za kusafirisha abiria.

Marufuku hiyo inatokana na mto huo kuongezeka maji na kina hivyo kuhatarisha usalama wa vyombo vinavyovusha watu na malizao.

Uamuzi wa kusitishwa huduma hiyo, inatokana na Kaimu Mkuu wa kivuko cha mto Kilombero, Mhandisi Faustin Magembe, kumwomba Mwenyekiti huyo kukifunga kwa usalama wa watu na mali zao.

Akitangaza kufungwa kwa kivuko hicho, Mwenyekiti huyo ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, alisema wananchi wa pande hizo watalazimika aidha kuzungukia mkoani Iringa au kubaki walipo hadi maji yatakapopungua.

Aidha alipiga marufuku matumizi ya kuvua au kuvuka kwa mitumbwi na kuagiza halmshauri ya Kilombero na Ulanga kutenga fedha za kutosha kununua boti zitakazotumika kuvushia abiria hususani kipindi hiki cha masika.


Akionesha kusikitishwa na kusombwa kwa kivuko hicho, Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanachi kuachana na uvuvi kipindi hiki hadi hapo hali itakapobadilika.


Kwa upande wake, Meneja wa Tanroads mkoa wa Morogoro, Doroth Mtenga, alisema kukatika kwa barabara baada ya kalavati kusombwa na maji shughuli yake itachukua muda kidogo kwani haiwezekani kwa hali iliyopo kurudishia karavati eneo hilotokana na kasi ya maji iliyopo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>