Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

OMPR yakana kula fedha za mfuko wa jimbo

$
0
0
Na Mwandishi wetu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema mkanganyiko uliojitokeza kuhusu fedha za majimbo hauhusiani na ofisi yake, kwani bado fedha hizo hazijaingizwa kwenye akaunti ya ofisi ya Makamu wa Pili.

Kauli ya Balozi Seif inakuja baada ya baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kutoka Zanzibar, kusema kwamba ofisi hiyo imezuia fedha hizo kwa sababu zisizoeleweka huku taarifa hizo zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema ni kweli kumekuwa na malalamiko ya aina hiyo yaliotolewa na baadhi ya Wabunge, lakini suala hilo haliihusu ofisi yake kwa vile fedha hizo baada ya kutolewa, haziingii moja kwa moja ofisini kwake.

Alisema ili fedha hizo ziweze kutolewa lazima kwanza zipite  Wizara ya Fedha Tanzania,  Ofisi ya Makamu wa Rais na baadae Wizara ya Fedha Zanzibarkabla ya kupelekwa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Alisema baada ya fedha hizo kufikishwa ofisini kwake, hupelekwa halmashauri za mikoa ambazo ndio wenye mamlaka ya kugawa fedha hizo majimboni.


Alisema madai kwamba ofisi yake imkalia fedha hizo hayana ukweli kwa sababu bado hazijatoka Wizara ya Fedha Zanzibar.

Alisema ni kweli fedha hizo zimeshafika Zanzibar, lakini kilichotokea ni kutokamilika kwa taratibu za fedha, baada ya kutokea matatizo.

Wabunge hao walidai wanapatwa na wasiwasi wa fedha hizo na kwamba huenda zimeliwa na ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.


Bunge hutoa shilingi milioni 25 kila mwaka kama fedha za maendeleo ya jimbo huku Baraza la Wawakilishi likitoa shilingi milioni 15 kwa kila Mwakilishi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>