Na Mwandishi Wetu.
Shirika la taifa la biashara Zanzibar ZSTC imevuka lengo na kununua ya tani 5345za za karafuu iliyokusudia kununua tani 3400 kwa mwaka 2013/2014.
Shirika la taifa la biashara Zanzibar ZSTC imevuka lengo na kununua ya tani 5345za za karafuu iliyokusudia kununua tani 3400 kwa mwaka 2013/2014.
Mkurugenzi muwezeshaji ZSTC Bi. Mwanahija Almasi Ali amesema mbali ya mafanikio hayo bado kuna changamoto kwa baadhi ya wakulima kuchanganya matende na makonyo na kuharibu sifa na ubora wa zao hilo katika soko la dunia.
Akizungumza na wadau wa zao la karafuu kwa wilaya ya Micheweni amesema ZSTC imevuka lengo hilo kunatokana na wakulima kufuata taratibu za shirika hilo.
Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Musini Pemba Juma Kassim Tindwa amewataka wakulima na wananchi kuendelea na vita vya kukomesha magendo ya karafuu kwa faida ya wakulima na taifa.
Akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa zao la karafuu wa wilaya ya chake amesisitiza wazanzibar kuongeza uzalishaji wa zao hilo pamoja na kurejesha ubora unaohitajika katika soko la dunia.