Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

NEC yatahadharishwa

$
0
0
Na Masanja Mabula,Pemba
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetakiwa kuwaandalia mazingira mazuri Masheha ili kuzuia kuingiliwa na wanasiasa wakati za zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Wakichangia mada kwenye mkutano uliowashirikisha wandishi wa habari na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kisiwani Pemba, washiriki wa mkutano huo walisema  Masheha wamekuwa wakiingiliwa na wanasiasa na kulazimisha watu wasio na sifa kuandikishwa.

Wandishi wa habari wa siku nyingi Ali Khatib Chwaya, aliitahadharisha Tume hiyo kwamba iwapo haitaandaa mazingira mazuri kwa Masheha zoezi hilolinaweza kuingia dosari kwa kuandikishwa watu waio na sifa.

“Kuna haja kwa Tume kukutana na wanasiasa hasa wa ngazi za chini ili kuwapa elimu ambayo itasaidia kutokuwepo na vitendo vya kuingilia madaraka ya sheha wakati wa zoezi hilo,na hii itasaidia kuleta ufanisi na mafanikio ya zoezi lenyewe,” alisema.


Naye Haji Nassor Mohammed akichangia kwenye mkutano huo, aliiomba Tume kuongeza uhamasishaji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwashirkisha ipasavyo wandishi wa habari kabla zoezi la uboreshaji halijaanza.

Alisema wanadishi wa habari ni kiungo muhimu katika kufanikisha zoezi hilo kutokana na kwamba wanakubalika, wanasikilizwa na wanaifikia jamii kwa wakati muafaka.

Akitoa ufafanuzi, Ofisa elimu ya mpiga kura na hahari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Salivatory Alute, alisema tayari Tume imeandaa mipango maalumu ya kukutana na wanasiasa ili kuwaleilimisha majukumu yaokwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema tume kupitia kitengo cha elimu ya mpiga kura na habari, imeanza kutoa elimu kwa wananchi kupitia vikundi vya sanaa pamoja na mikutano ya hadhara inayowashirikisha wananchi.

Mapema akifungua mkutanao huo, Kamisha wa tume hiyo, Jaji Mstaafu John Mkwawa, aliwaomba wandishi wa habari kutumia vyema taaluma yaokatika kuwafikishia wananchi ujumbe na elimu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema tume imekuwa ikitumia vyombo vya habari katika kuiunganisha na wadau mbali mbali wa uchaguzi wakiwemo wapiga kura na kuongeza kwamba wandishi wa habari wapo karibu na jamii.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>