Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wachungaji Morogoro wapiga marufuku vijana wa Kisukuma kutembea na fimbo

$
0
0
Na Farida Msengwa,Morogoro

WACHUNGAJI wa jamii ya kisukuma wamepigwa marufuku  kutembea mitaani na fimbo kutokana na baadhi yaokuzitumia vibaya kwa michezo ambayo wakati mwingine husababisha mauaji.

Onyo hilo limetolewa na Ofisa tarafa wa Ngoheranga,Conrad Mzwalandili, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa vijiji vya Ngoheranga na Ihowanja wilayani Ulanga na kusema kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu athari ya fimbo pamoja na ngoma.

Alisema imebainika baadhi ya vijana huchapana hadi kusababisha mauaji na tayari zaidi ya fimbo sabini zimekamatwa, huku akiwataka wananchi wa eneo hilo kutembea kwa kujiamini katika Tanzania huru, badala ya kutumia fimbo ambazo zimegeuka silaha.

Alisema wamepiga marufuku ngoma aina ya sagulaga, ambayo imekuwa ikiwadhalilisha mabinti wakiwemo wanafunzi,ambao vijana hata zaidi ya  100  humkimbiza binti bila kujali ni mwanafunzi ama vinginevyo na kumfanyia matendo yasiyo faa.

Awali wananchi wa kijiji cha Ihowanja, Luminicu Ngonyani, Anastasius Ngaliwa na Frank Kufakwenda katika mkutano wa hadhara, waliilalamikia serikali ya kijiji chao kugawa  maeneo ya ardhi kiholela kwa wageni kutoka nje, huku fedha zinazopatikana wakiwa hawajui matumizi yake.


Hata hivyo , Mwenyekiti wa kijiji cha Ihowanja, Yonas Ngonyani, alisema wanaolalamikia kwa kufanya matumizi mabaya ya  fedha za kijiji wengi ni  kutoka vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakiwashawishi wananchi kushiriki kazi za kujitolea kwa maendeleo yao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>