Na Mwandishi wetu
WANAJESHI watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamefariki katika ajali ya gari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya JWTZ Upanga, ajali hiyo iliwahusisha wanajeshi watano.
Taarifa hiyo ilisema ajali hiyo ilitokea baina ya Rwindi na Kanyabayoga ikilihusisha gani lenya namba UN 47089 aina ya Leyland Ashock lililokuwa kwenye msafara kutoka
Gari hilo lilikuwa na wanajeshi watano miongoni mwao watatu,walifariki dunia papo hapo.
Wanajeshi waliofariki ni Private Mohamed John Mbizi, Private Vasco Adrian Msigala na Private Ally Salum Jumanne.
Aidha wanajeshi wawili walipata majeraha, ambao walichukuliwa kwa helikopta kwenda Goma kwa matibabu zaidi.
Waliojeruhiwa ni Private Emily Edward Lyombe na Private Haji Hassan Amme.
Taratibu za kuirejesha miili ya wanajeshi hao nyumbani kwa mazishi zinaendelea.