Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Nzowa kuwashughulikia vigogo wauza unga

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, Arusha
KAMANDA wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (SACP) Godfrey Nzowa, ameapa kutokomeza wimbi la uingizaji na usafirishaji wa dawa za kulevya huku akisisitiza kupambana  na vigogo wanaotajwa kuhusika na mtandao huo.

Alitoa wito kwa jamii kuunga mkono jitihada zake za kupambana na mtandao huo, aliodai ni hatari, kwa kutoa taarifa za siri ili hatua zaidi za kukabiliana na uhalifu huo zichukuliwe.

Kauli hiyo aliitoa jijini hapa wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari,ambapo alisisitiza kutokomeza mtandao huo kabla hajasitaafu kazi katika kipindi kifupi kijacho.

“Kwa sasa mimi ni mstaafu ila nimekuwa nikiongezewa muda kutokana na unyeti wa kitengo hiki, hata hivyo kwa sasa najiandaa kustaafu rasmi,ila nataka kabla sijastaafu niwe nimeufuta mtandao huu,hata hivyo, nimejitahidi kujenga mtandao wa mawasiliano katika nchi  mbalimbali duniani unaosaidia kufanikisha ukamataji wa wa wasafirishaji dawa za kulevya,” alisema.

Adha alisema Watanzania wamekuwa vinara wa kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya nchini na nje ya nchi huku takwimu zikionesha  kati ya kesi 98 zilizoko mahakamani idadi kubwa ya washtakiwa ni Watanzania.


“Kwakweli Watanzania ndio wanaoongoza kwenye biashara hii, wakifautiwa na raia wa Nigeria,Pakistan na Waasia,” alisema.

Alisema kikosi chake kimepiga hatua kubaini mbinu zinazotumiwa na wahalifu hao wakati wa usafirishaji,ikiwemo kuwatumia akina mama wajawazito,kuweka sehemu za siri,kufunga kwenye vifungashio vya bidhaa halali pamoja na njia mpya inayotumika kwa sasa ya kusafirisha mali ghafi badala ya kete halisi.

Alisema wakati anaongoza kitengo hicho mwaka 2006, alikuta kilo mbili pekee za dawa aina ya heroin zilizokamatwa, lakini hadi  kufikia Februali 2014, wamefanikiwa kukamata hadi kilo 200.5 za heroin idadi ambayo ni kubwa kukamatwa kwa mkupuo mmoja.

Hata hivyo, alisema kazi hiyo ni ngumu na inahitaji ujasiri wa hali ya juu kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutishiwa kuuawa na  rushwa ya fedha.

Aliongeza kuwa ofisi yake inafuatilia kwa makini taarifa zozote zinazotolewa na raia wema hasa baada ya kuwepo habari kuwa kuna mtandao wa vigogo wanaojihusisha na uuzaji nausafirishaji  wa dawa hizo huku akisisitiza kuwa hakuna atakaye salimika hata kama awe na cheo gani.

“Tunathamini sana taarifa zinazoletwa kwetu na zinatusaidia kuwanasa wahalifu,  hapa nchini tumepata taarifa nyingi za watu  wakubwa ila bado tunafuatilia kwa kina muda si mrefu utasikia tu tumekamata ila tunashangaa kwanini hawafungwi?’’alihoji.

Akizungumzia rekodi za ukamataji wa dawa hizo, alisema idadi kubwa ya dawa zinazokamatwa  ni aina ya heroin zikifuatiwa na cocaine.

Alisema mwaka 2010 walikamata kilo195 za heroin mkoani Tanga huku jijini Dar es Salaam, zikikamatwa kilo 179.

Alisema mwaka 2012 mkoani Lindi walikamata kilo 211 na mwaka  2013 walikamata kilo 50 jijini Dare es Salaam.


Alioa rai kwa askari polisi wawe waadilifu pindi wanapowakamata watuhumiwa na kuacha tamaa zisizo kuwa na tija ili weweze kufanikiwa kutokomeza mtandao huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>