Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

DC magharibi aahidi kumaliza migogoro ya ardhi

$
0
0
Na Hafsa Golo
MKUU wa wilaya ya magharibi  Unguja,Ayoub Mohammed Mahamoud, amesema  anakusudia kulipatia ufumbuzi tatizo  sugu la ndani ya wilaya ya magharibi ambalo limeonekanwa kudumu kwa muda mrefu.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo mara  baada ya hafla fupi ya kumpongeza kuteuliwa kushika nafasi hiyo, katika hafla iliyofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa Vuga.

Alisema migogoro ya ardhi katika wilaya hilo ni makubwa ambapo  kuna zaidi ya kesi 27 zilizopo mezani zinazohitajia kusuluhishwa na kesi zaidi ya 580 tayari zipo mahakamani.

Alisema migogoro hiyo imekuwa endelevu kutokana na wimbi kubwa la ukuaji wa idadi ya watu ambapo, alisema mwaka 2002 watu walikuwa wastani wa 180,000 ambapo hivi sasa imefikia wastani wa watu 370,645, kati ya watu 568,688 waliomo mkoa wa mjini magharibi.

Alisema kutokana na ukubwa wa migogoro hiyo italazimika kulitazama suala hilo kwa ukaribu zaidi kwa kulitathimini kwa kina ili kuondosha mivutano hiyo ambayo imekuwa kukileta matabaka miongoni mwa wananchi.


“Nitakutana na taasisi za ardhi,kukaa pamoja na kamati za kijamii, masheha, wazee,vijana,asasi za kiraia na  wanasiasa kujaribu kulitafutia ufumbuzi suala hili,” alisema.

Akizungumzia amani na utulivu, alisema vitendo vingi vinavyosababisha uvunjifu wa amani vimekuwa vikitokea katika wilaya hiyo hivyo ni vyema kushirikiana pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vitendo hivyo vinatoweka.

Alisema jambo jengine ambalo amelikusudia kuliimarisha ni kuileta jamii pamoja na kushirikiana katika masuala ya kijamii ili ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi uweze kuwanufaisha wote.

Kwa upande wake aliekuwa Mkuu wa wilaya ya magharibi, Mussa Hassan Takrima, alimshauri kuwa makini juu ya masuala ya ardhi kwani yamekuwa kero kubwa kwa wananchi.


Mkuu wa Mkoa wa mjini magharibi, Abbdala Mwinyi, alisema alimshauri mkuu huyo wa wilaya kutumia zaidi hekma za busara wakati anapotekeleza majukumu yake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>