Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mama Asha ahimiza maskini kusaidiwa

$
0
0
Na Mwantanga Ame
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,mama Asha Suleiman Iddi, amewataka wananchi kuwasaidia watu wenye hali duni ili kuwawezesha kukabiliana na maisha yao.

Aliyasema hayo jana wakati akikabidhi misaada ya vifaa mbali mbali zikiwemo nguo, vitu vya nyumbani, vitabu vya wanafunzi, vitabu vya dini na vyakula na mafuta, kwa wakazi wa vijiji vya Matemwe Mbuyu Tende, Kijini, Mvuleni na Mgonjoni.

Akizungumza kwa niaba ya mama Asha, Katibu wa CCM mkoa wa kaskazini Unguja,  Ame Omar Mkadam, alisema Zanzibar bado kuna watu wanahitaji kupatiwa misaada ili kubadili maisha yao.

Alisema  Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, katika uhai wake alipenda kuona maisha ya Wazanzibari yanakuwa katika usawa na ndio maana aliwaachia usia wa kugawana kidogo kwa alienacho lakini waenee.

Kutokana na falsafa hiyo, alisema,ameamua kuwasaidia wananchi wa vijiji hivyo ili kufuata maneno ya hekima kivitendo ya kiongozi huyo.


Alisema ni jambo ka kusikitisha kuona baadhi ya watu wenye vipato wanashindwa kuwasaidia watu wenye mazingira magumu jambo ambalo linaondoa utamaduni wa kusaidiana.

Aliwaahidi wanavijiji hao kuendelea kushirikiana nao kwa kuwasaidia kila pale atakapoona upo umuhimu wa kufanya hivyo kwa vile ni sehemu ya kuendeleza sera ya CCM.

Baadhi ya wana vijiji hao, wakitoa shukrani zao, walimpongeza mama Asha kwa jitihada anazofanya kuwapatia misaada ya kibinaadamu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>