Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

OT yatoa sarafu ya sh.500

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa sarafu ya shilingi 500, ambayo itaanza kuingia kwenye mzunguko mwezi Oktoba mwaka huu.

Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu, Emmanuel Boaz, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema sarafu hiyo mpya ina umbo la duara na michirizi pembezoni, rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini ya chuma na nikeli.

Kwa mbele ina sura ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu  Sheikh Abeid Amani Karume na kwa nyuma ina picha Nyati akiiwa mbugani.

Aidha ina alama ya usalama iitwayo ‘latent image’ iliyopo upande wa nyuma  ambayo ni kivuli kilichojificha, kinachoonesha thamani ya sarafu ‘500’ au neno BOT inapogeuzwageuzwa.

Sarafu hiyo itatumika sambamba na noti zilizopo sasa za shilingi 500 mpaka  zitakapokwisha kwenye mzunguko.

Alisema sarafu  hiyo imetolewa kwa kuzingatia kwamba  noti ya shilingi mia tano ndiyo inayotumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila siku ya wananchi wengi kuliko noti nyingine yoyote.


Hali hiyo husababisha  noti hiyo kupita kwenye mikono ya watu wengi katika kipindi mfupi na kuchakaa haraka.


Pia hukaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe zinapokuwa zimefikia ukomo wake. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>