Na Mwandishi wetu
TUME ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba wahisani wa shughuli za UKIMWI wamejitoa kufadhili shughuli hizo kuanzia mwaka ujao.Hata hivyo, Tume hiyo imesema baadhi ya wahisani ambao wanajitoa kwenye ufadhili ni kutokana na miradi wanayoifadhili kuisha muda wake au kubadilika vipaumbele.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume hiyo, Dk. Fatma Mrisho, imeitolea mfano serikali za Canada na Denmark ambazo zimekuwa zikisaidia programu za UKIMWI kwenye mamlaka za serikali za mitaa na jamii ambapo mradi wao unaisha 2016/17.
Hata hivyo alisema serikali ya Denmark bado ina nia ya kuendelea kusaidia shughuli za UKIMWI, baada ya mradi huo kuisha.
Mwenyekitu huyo alisema utekelezaji wa shughuli za UKIMWI Tanzania umekuwa ukipata ufadhili wa fedha kutoka serikali ya Tanzania na serikaliza nchi Marafiki.
Alisema programu zinazotekelezwa hufuata mkakati wa taifa wa kudhibiti UKIMWI (NMSF) na mpaka sasa kuna uhakika waf edha za UKIMWI kwa miaka mitano ijayo.
Alisema serikali za nchi Marafiki wamekuwa wakisaidia shughuli za UKIMWI kwa mtindo wa miradi ambayo ni ya muda mfupi.
Alisema wahisani wakubwa wa shughuli za UKIMWI ni serikali ya Marekani na Mfuko wa Dunia wa Magonjwa ya UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria.
Wahisani hao wawili wanatoa kiasi cha asilimia 80 ya fedha za UKIMWI nchini na ndio wanaofadhili programu ya tba ya UKIMWI nchini na programu zao bado zinaendelea na hawajatangaza kujitoa.
Alisema serikali iko katikahatua za mwisho za kuanzisha Mfuko wa UKIMWI Tanzania ambao utachangiwa na serikali, wadau wengine nchini pamoja na wadau wa Maendeleo.