Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Shein, Akutana na Mfalme wa Uholanzi.

$
0
0
Na Said Ameir, Uholanzi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewasili nchini Uholanzi kuanza ziara rasmi ya siku tano nchini humo kufuatia mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mark Rutte.

Juzi Dk. Shein alitembelea bandari ya Rotterdam ambapo baadae alifanya mazungumzo na makampuni yaliyo katika sekta ya miundombinu ya usafiri wa bahari.

Jioni alikutana na Mfalme wa Uholanzi, Willem Alexander na baadae kuhudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshma yake.

Leo atakutana na Waziri wa Biashara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Lilianne Ploumen na pia atafanya mazungumzo na wadau katika sekta ya Nishatina baadae kutembelea makao makuu ya kampuni ya mafuta ya Shell.

Kesho asubuhi Dk. Shein atakutana na Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte.

Baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uholanzi, Rais wa Zanzibar atatembelea kampuni ya vifaa vya uchunguzi wa maradhi ya sakura ambako atabadilishana mawazo juu ya masuala ya afya kati ya Zanzibar na Uholanzi.

Siku hiyo baadae mchana atatembelea bandari ya Scheveningen ambako atakutana na wananchama wa Muungano wa wadau katika sekta ya uvuvi na kukutana pia na uongozi wa kampuni ya usindikaji na uuzaji wa mazao ya bahari nchini humo.

Baadae jioni atakutana na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi mjini The Hague.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Schiphol mjini Amsterdam Dk. Shein alipokelewa na Mwakilishi wa Mfalme wa Uholanzi, Kamanda Juan Irausquin, Naibu Mkurugenzi wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, Micheal Rauner, Balozi wa Uholanzi nchini Jaap Fredericks, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Balozi Diodorus Kamala na Frans Hakkenberg, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uholanzi.

Katika ziara hiyo Dk. Shein amefuatana Waziri Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati,Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Rashid Seif Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Kombo Haji.

Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini tarehe 1 mwezi ujao.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles