Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Lukuvu Wabunge Wamo Orodha Wanaodaiwa Kuingiza Unga.

$
0
0
Na Mwantanga Ame, Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Bunge, William Lukuvi, amesema Wabunge ni miongoni mwa wanaotajwa kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya na serikali inalazimika kufanya uchunguzi.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya Wabunge waliotaka kujua ni kwa nini serikali imekuwa na kigugumizi kuwataja wasafirishaji wa dawa hizo.

Baadhi ya Wabunge ambao walihoji hilo ni pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israeli Natse na Mbunge wa Viti maalum, Capline Magige, ambapo wote walitaka kujua hatua za serikali katika kupambana na dawa hizo.

Pia Wabunge hao waliiomba serikali kueleza jinsi inavyohifadhi dawa hizo baada ya kesi za washtakiwa kumalizika.

Alisema baada ya dawa hizo kuthibitishwa na mshitakiwa kutiwa hatiani huteketezwa.

Lukuvi alisema wabunge wengi wemetajwa katika orodha ambayo serikali inayo.

Alisema kazi ya serikali sio kukamata kila mtu anayetajwa kabla ya kuyafanyia uchunguzi.

Alisema wanafanya uchunguzi kwa kuhofia serikali kuaibika kwa kupeleka mahakamani watu wasiojihusisha na biashara hiyo.

Alisema kama kuna mtu mwenye majina ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na uuzaji wa dawa za kulevya wanaweza kuyapeleka serikalini ili kufikishwa mbele ya bunge.

Alisema hivi karibuni kuna baadhi ya watumishi wamaehusishwa na uingizaji wa dawa za kulevya na mamlaka husika imekuwa ikifanya kazi kuona nani anaehusika.

Alisema kilo 873.8 za heroin zimekamatwa huku watuhumiwa wa matukio hayo walifikia 2,486 wakati cocaine zilifikia kilogramu 373.57 na watuhumiwa waliohusika ni 836.

Alisema Watanzania 247 wamekamatwa katika nchi mbali mbali wakisafirisha dawa za kulevya kuanzia mwaka 2008 hadi Julai 2013.

Alisema nchi hizo ni pamoja na Mauritius, Falme za Kiarabu, China, Pakistan, Brazil na Afrika Kusini huku raia wa kigeni 31 wanashikiliwa katika magereza mbali mbali ya Tanzania baada ya kukamatwa wakiwa na dawa hizo.
Raia hao ni kutoka Iran, Pakistan, Nigeria, Senegal na Afrika Kusini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>