Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Nchi 17 Kushiriki Kongamano la Ustaarabu wa Kiislam Zanzibar.

$
0
0
Na Mwashamba Juma
WASHIRIKI zaidi ya 170 kutoka mataifa 17 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano la kimataifa la ustaarabu wa kiislamu kwa nchi za Mashariki mwa Afrika, linalofanyika Zanzibar kuanzia Septemba 2-4 katika hoteli ya La Gemma Della East, Nungwi.

Kongamano hilo lenye lengo la kuitangaza Zanzibar kimataifa hasa katika nyanja za utalii na masuala ya utafiti na taaluma kupitia Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA), linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na kufungwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilali.

Kongamano hilo litawakutanisha wahadhiri na wataaalamu mbambali wa historia, utamaduni wa kiswahili na kiarabu pamoja na dini ya Kiislam na linaandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Kumbukumbu na Nyaraka ya Oman na SUZA.

Nchi zitakazoshiriki kongamano hili ni Burundi, Kenya, Tanzania Bara, Uganda, Comoro, Zimbabwe, Algeria, Lebanon, Misri, Tunisia, Iraq, Oman, Uturuki, Yemen, India, Uingereza,Ujerumani na wenyeji Zanzibar.

Aidha washiriki wengine ni pamoja na wahadhiri kutoka Vyuo Vikuu na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kutoka Jumiya ya Maendeleo ya Kiislam Duniani (OIC) pamoja na Waziri wa Habari wa Oman, Dk. Abdulmunim bin Mansour bin Said al Hasani.

Mkutano huo wa kimataifa ni wa pili baada ya ule wa Kampala, Uganda uliofanyika mwaka 2012 na kuchaguliwa Zanzibar kufanyika mkutano huo kunatokana na historia yake na mahusiano ya karibu na mataifa ya kiarabu duniani.
Washiriki wa mkutano huo wanatarajiwa kuanza kuwasili nchini leo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>