Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kesi za Meli Zilizovua bila ya Ruhusa Tanzania Yaendelea.

$
0
0
Na Mwantanga Ame
SERIKALI imesema bado inaendelea kulifanyia kazi suala la kampuni mbili za uvuvi za Taiwan, zilizokamatwa baada ya kudaiwa kuvua uvuvi haramu katika maji ya bahari ya Tanzania.

Hatua hiyo ya serikali, huenda ikachukuliwa baada ya Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Robert Manumba, kuithibitishia serikali kwamba kampuni hiyo ilifanya makosa kwa kuvua bila ya leseni katika maji ya Tanzania.

Kauli ya Manumba inakuja baada ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu, kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya IOTC, ambayo nayo ililiweka hadharani katika mitandao yao inayotaka kufanyika uchunguzi juu ya suala hilo.

Kadhia hiyo iliihusisha meli ya HWA KUU namba. 168 inayomilikiwa na kampuni ya meli ya Chang WC, na Hasiang FA 26 inayomilikiwa na kampuni ya Marina Marine Limited.

Akizungumza na Zanzibar Leo, Naibu Waziri wa Wizara ya Uvuvi, Mohammed Said Dimwa, alisema tayari suala hilo limeshakamilika kwa vile muda uliowekwa kisheria kushughulikia kesi za aina hiyo umefikia kikomo.

Alisema kutokana na kukamilika kwa kazi hiyo, tayari kuna mapendekezo yaliyotolewa na vyombo husika katika kushughulikia kesi za aina hiyo, ambayo hivi sasa serikali inaangalia namna bora ya hatua za kuchukuliwa.

“Ni juzi tu tumepata ripoti ya DCI Manumba, sasa serikali itakaa na kuangalia njia ya kutumia kati ya mapendekezo yaliomo kisheria,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa sheria inayosimamia masuala ya uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania, inataka kuwepo majadiliano kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wahusika na kama kutakosekana muafaka basi nchi wanachama watapiga kura aidha kuziorodhesha meli hizo au laa.

Kutokana na matakwa hayo ya kisheria, Dimwa alisema baada ya kesi hizo kuripotiwa katika Jumuiya ya IOTC, kikao kilifanyika mwezi Mei nchini Mauritius, ambapo serikali ya Tanzania ilipewa nafasi ya kutoa ushahidi wake.

Alisema katika ushahidi huo, Tanzania ilifanikiwa kuzitia meli hizo mbili hatiani.

Alisema meli ya Hwa Kun yenye namba 168, ilidaiwa kuingia katika maji ya Tanzania na kufanya shughuli zake ikiwa na leseni 859 ambayo ilielezwa kutolewa Tanzania, lakini ilibainika haina ukweli, kwani hakuna leseni namba hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

Matokeo hayo yalipekwa Mamlaka ya Uvuvi nchini Taiwan, kufanyiwa uchunguzi huku Mamlaka ya uvuvi ya nchini Seychelles, nayo imekataa kutoa leseni yenye namba 970, ambayo nayo ilidaiwa kutolewa na Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu nchini.

Alisema katika sakata hilo pia serikali ya Tanzania ilipokea leseni namba 8 kutoka mamlaka ya nchini Seychelles, ambazo zilibainika kuwa ni feki baada ya kuonesha jina na picha ya Ahmeid Al Shaibani ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Zanzibar marine Product Ltd, ambaye ni mwakilishi wa meli hizo Tanzania.

Vile vile, Naibu huyo alisema katika uchunguzi huo pia ulibaini saini zenye kuonesha jina la Chando, ambae ni ofisa mdhibiti wa mamlaka hiyo wakati sio muhusika katika utoaji wa leseni.

Akiendelea alifahamisha kuwa thamani ya leseni ambazo ziliorodheshwa kuwa ni za udanganyifu kutokana na kughushiwa kwa dola za kimarekani 104,800 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 167,680,000.

Kutokana na kuwepo hali hiyo, Naibu Waziri huyo, alisema tayari DCI Manumba amekamilisha uchunguzi wake na hivi sasa serikali inafikiria namna ya kulifanyia kazi suala hilo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>