Na Hafsa Golo
BENKI ya Exim ya China itaipatia Zanzibar mkopo kwa ajili mradi wa ujenzi wa bandari ya Mpiga duri.
Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga.
Alisema mazungumzo kati ya watendaji wa serikali ya Zanzibar na China juu ya kuanza mradi huo zimefikia muafaka.
Alisema Meneja Mkuu wa Idara ya mikopo nafuu katika benki hiyo,Wang Fde alisema wapo tayari kutia msukumo ili Zanzibar iweze kuwa na bandari ya kisasa yenye kujitosheleza.
Alisema pia kuna miradi mingine miwili imezungumziwa ikiwemo matumizi ya mkongo wa taifa kwa upande wa afya na kuongeza ukusanyaji mapato Zanzibar.
Alisema mradi huo utaimarisha afya hasa katika suala zima la utambuzi wa maradhi ya binaadamu ili kurahisisha matibabu.