Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Haroun:Wasomi timizeni wajibu wenu

$
0
0
Na Juma Khamis
WAZIRI wa Nchi (OR), Kazi na Utumishi wa Umma, Mhe.Haroun Ali Suleiman, ametoa changamoto kwa wasomi kuandika machapisho mbalimbali ya kitaalamu, akisema haiwezekani msomi mwenye shahada ya uzamivu (PhD) kukaa miaka mitano bila kuandika chochote.
Alisema kutokuandika ni kasoro kubwa na msomi wa aina hiyo atakuwa haitendei haki taaluma yake.
Alikuwa akizungumza katika fainali ya mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi, yaliyofanyika kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Vuga.
Aidha alipongea wazo la kuandaa mashindano hayo, akisema yanawajengea wanafunzi uwezo wa kujiamini na kuwa viongozi wa baadae.
Alisema serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya kufundishia na maslahi ya watendaji wakiwemo walimu hatua kwa hatua.
Hata hivyo, aliwataka walimu kuwajibika na kufundisha kwa ari kujenga ustawi bora wa jamii ya kizanzibari.
Alichangia shilingi 300,000 kwa mshindi wa kwanza na kiwango kama hicho kwa mshindi wa pili pamoja na kuahidi kuchangia shilingi 2,000,000 wakati mashindano hayo yatakapoandaliwa tena mwaka 2014.

Mapema Makamu Mkuu wa SUZA, Prof. Idris Ahmada Rai, alisema mdahalo kwa wanafunzi wa elimu ya juu unawafanya wanafunzi wajiamini wanapozungumza  mbele za watu, hivyo unapaswa kuendelezwa.
Alivipongeza vyuo vikuu vyengine kwa kuunga mkono wazo la kuandaa mdahalo huo na kushiriki katika hatua zote.

Mdahalo huo ulivishirikisha vyuo vya SUZA, Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) Tunguu, Chuo cha Uongozi wa Fedha (ZIFA) na Chuo Kikuu cha Elimu Kishiriki Chukwani, ambapo SUZA kimeshinda kwa kupata asilimia 84 dhidi ya asilimia 74.8 za ZIFA. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>